- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Idadi ya watumiaji wa simu nchini Tanzania wafikia milioni 40.173
Dar es salaam: Matumizi ya Simu za mkononi nchini yaongezeka kwa zaidi ya asilimia 66% toka mwaka 2005 mpaka 2016, MKURUGENZI wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Kilaba, amesema Tanzania imeendelea kushuhudia maendeleo makubwa katika sekta ya mawasiliano ambapo kwa sasa "laini" za simu za kiganjani zinatumika zimefikia 40,173,783 hadi kufikia Desemba mwaka jana (2016).
Kwa mujibu wa Mhandisi Kilaba, idadi hiyo imeongezeka kutoka ile ya mwaka 2005 ambapo takwimu zinaonesha kuwa laini za simu zilizokuwa zikitumika zilikuwa 2,963,737. Maana yake ni kwamba katika kipindi cha miaka 11 kumekuwa na ongezeko la laini mpya 37,210,046.
Mhandisi Kilaba alitoa takwimu hizo leo (Februari 22, 2017) wakati wa uzinduzi wa programu ya elimu kwa umma kuhusu HUDUMA YA KUHAMA MTANDAO MMOJA WA SIMU kwenda MTANDAO MWINGINE BILA KUBADILI NAMBA YA SIMU. Tukio hilo la uzinduzi limefanyika katika ofisi za TCRA makao makuu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari nchini.
"Nchji yetu kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani kote imeshuhudia ukuaji wa kasi wa sekta ya mawasiliano ambao umechangia sio tu katika kuboresha maisha ya wananchi kijamii na kiuchumi lakini pia katika pato la taifa husika. Ukuaji wa sekta ya mawasiliano hapa kwetu umechangiwa na kuwepo kwa sera, sheria, kanuni na mfumo mzuri wa utoaji leseni za huduma za mawasiliano," alisema Mhandisi Kilaba.
Kuhusu kuhama mtandao
Akizungumzia kuhusu huduma ya kuhama kutoka mtandao wa simu mmoja kwenda mtandao mwingine, Kilaba alisema; "Ni huduma inayomwezesha mteja kubakia na namba yake (tarakimu zote 10) bila kujali anatumia mtandao gani na pindi anapoamua kuhamia mtandao mwingine basi anahama na namba yake ya nzima, hivyo hana haja ya kusumbua kuwataarifu watu wake wa karibu β marafiki, familia na wafanyakazi wenzake au washirika katika shughuli zake kwamba amebadilisha namba kwani namba inabakia ile ile."
Alisema huduma hiyo katika Afrika imeanzishwa nchini Misri, Kenya, Sudani, Afrika Kusini, Ghama, Nigeria, Senegal na Morocco na kwamba nchi nyingine ambazo ni pamoja na Rwanda na Namibia zipo katika mchakato wa kuanzisha huduma ya namna hii.
Alizitaja faida za huduma hiyo kuwa ni pamoja na kuongeza ushindani kwenye sekta ya mawasiliano na hivyo kuwa kichocheo cha utoaji huduma bora kwa kuwa kama huduma za haziridhishi basi wateja husika watahama na namba zao kwenda mtandao mwingine.
Alibainisha faida nyingine akisema; "Kumpa uhuru mtumiaji wa huduma za simu za viganjani kuchagua mtoa huduma ambaye anaona anatoa huduma bora zaidi, huduma nzuri kwa wateja na ana ubunifu katika kutoa huduma zake."