- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HUENDA RAIS KIKWETE BADO ANAUSHAWISHI MKUBWA KULIKO MAGUFULI
Dar es salaam: Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete Jana Jumapili Julai 8, 2018 amelikuwa kivutio cha wananchi wengi katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu Sabasaba baada ya wananchi wengi kumfuata kila banda alilokuwa akitembelea kwa maana ya kujionea.
Watu walishuhudia baadhi ya wananchi, wakiacha kutembelea mabanda mbalimbali ya biashara na kumfuata rais huyo mstaafu.
Saa nane mchana Kikwete alikuwa kwenye banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), huku nje ya banda hilo kukiwa na idadi kubwa ya wananchi, wengi wakiwa na shauku ya kumuona.
Hali ilikuwa hivyo katika kila banda alilotembelea, licha ya wananchi hao kuzuiwa na askari walizidi kuongezeka kadri kiongozi huyo mstaafu alivyokuwa akitembelea maeneo mbalimbali.
Kuna baadhi ya kauli za wananchi zilizokuwa zinasikika wakati wakitembea kuonesha BADO wanamuhitaji Rais huyo
“Baba tumekukumbuka uko wapi baba,” walisikika wakisema baadhi ya wananchi hao.
Akizungumza katika maonyesho hayo, Kikwete ameishauri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuwawezesha wafanyabiashara kupenya katika soko la kimataifa.
“Ni jukumu lao kuwasaidia wafanyabiashara kufikia soko la kimataifa kwa sababu biashara ni nzuri na zina ubora,” amesema.
Aliwataka wafanyabiashara wa ndani kujifunza kwa wafanyabiashara waliopiga hatua zaidi.