Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 10:29 pm

News: Hospitali ya LONGIDO yakbidhiwa vifaa Tiba na PPF

ARUSHA: Taasisi ya mfuko wa hifadhi ya jamii PPF leo umekabidhi vifaa tiba kwenye Kituo cha afya cha LONGIDO kilichopo mjini Arusha, Hatua hiyo ya PPF kukabidhi vifaa hivyo ni utamaduni wa Taasisi Hiyo Katika kuahaikikisha wanakuwa sehemu ya kusaidia jamii nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo,(wanne kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia Afya), Dkt. Zainabu Chaula,(kulia), Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Daniel Chongolo, (wapili kushoto), na viongozi wengine, wakiangalia kitanda cha kujifungulia wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na PPF.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(watatu kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (wapili kushoto), Viongozi wa Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Longido, wakitembelea wodi ya wagonjwa ya Kituo cha Afya Longido, ambapo ni moja kati ya vituo vilivyonufaika na msaada huo wa vifaa tiba kama sehemu ya mchango wa PPF kwenye Jamii.