- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HESLB KUTUMIA VITAMBULISHO VYA TAIFA KUREJESHA MKOPO
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB), imesema kuwa uwepo wa vitambulisho vya Taifa, nchini utasaidia pakubwa bodi hiyo katika kuwabana wanufaika wa mikopo ili waweze kurejesha kwa wakati mikopo yao.
Bodi ya mikopo imekuwa ikipata shida sana kutafuta njia sahihi ya kuwabana wanufaika wa miko hiyo pindi wapatapo ajira kwenye makampuni na taasisi mbalimbali.
Akizungumza na East Africa Radio, hii leo Mkuu wa Mawasiliano ya Bodi hiyo, Omega Ngole amesema kuwa wanaufaika wengi wamekuwa wakijificha pindi wanapohitimu elimu hiyo ya juu, hivyo kuisababishia hasara bodi na kupelekea wanafunzi wengi kukosa mikopo.
Aidha Omega ameongeza kuwa makato hayo ya asilimia 15 yanayopingwa na baadhi ya wadau nchini, yamefanya bodi ikusanye marejesho ya Shilingi Bilioni 18.9 ndani ya mwezi mmoja.