- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Hatimae Rais wa Korea kusini Ameng'olewa madarakani kwa lazima
Seoul: Kilio cha wakazi wengi wa Korea Kusini kumtaka Rais wa nchi hiyo Bi Park Geun-hye kuondoka madarakani kimehitiimishwa na Mahakama ya juu nchini Korea Kusini ambayo imeunga mkono uamuzi wa bunge wa kumuondoa rais wa taifa hilo Park Geun-hye mamlakani.
Mahakama hiyo ya kikatiba imesema kuwa bi Park alikiuka sheria na kuharibu demokrasia nchini Korea.
Park ambaye ndio mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini humo alihusishwa na kashfa ya kujipatia fedha kwa njia za ufisadi kutoka makampuni makubwa nchini humo na rafikiye mkubwa Choi Soon-Sil.
Bi Park huenda akakabiliwa na mashataka ya uhalifu.
Uamuzi huo ulipokelewa kwa shangwe katika maeneo mbali mbali yalio na wapinzani wa rais huyo.
Lakini wafuasi wake pia walionekana na kumekuwa na mzozano kati ya makundi hayo mawili.
Uchaguzi wa urais sasa utafanyika katika kipindi cha siku 60.
Bi Park alikuwa amesimamishwa kuhudumu kama rais tangu mwezi Disemba huku waziri mkuu wa taifa hilo akichukua majukumu ya kuongoza taifa.
Bi Choi wakati huohuo ameshtakiwa kwa kuchukua hongo kwa madai ya kuyashinikiza makampuni makubwa kumpa pesa huku akiahidi kwamba kampuni hizo zitapendelewa na serikali.