November 23, 2024, 3:46 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Hatimae CIA watoa Report Rasmi inayohusu Udukuzi kwenye uchaguzi mkuu wa Marekani
Washington: Ripoti iliyotolewa na maafisa wa C.I.A Marekani ilisema kuwa Urusi ilikusudia kuchochea ili wananchi Wamarekani wakose imani katika katika demokrasia ya nchi yao na pia kumdhalalisha mpinzani wa Bwana Trump, Bi Hillary Clinton katika uchaguzi mkuu ulio fanyika mwishoni mwa mwaka jana.
Ripoti hiyo kwa mara ya kwanza inamshirikisha Bwa Putni katika shughuli za udukuzi moja kwa moja katika uchaguzi wa Marekani.
Makamu wa Rais Mteule, Mike Pence, alisema baadaye kuwa Bwana Donald Trump baadaye atachukua hatua kali dhidi ya udukuzi wo wote unaokabili Marekani kutoka kwa taifa lo lote lile.
Baada ya kukutana na maafisa wa ujasusu, Bwana Trump alisema kuwa amejifunza mengi kuhusiana na shughuli za udukuzi lakini akakanusha kuwa udukuzi huo ulibadili mkondo wa matokeo ya uchaguzi wa Urais kwa njia ye yoteAFP