- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HALIMA MDEE NA JOHN MNYIKA WAMKALIA KOONI WAZIRI WA FEDHA
Dodoma: Mbunge wa Kawe Mh Halima Mdee na Mbunge wa Kibamba John Mnyika (wote Chadema) Leo June 5 wamembana vyakutosha Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango wakitaka kujua zipo wapi fedha zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za 1.5 trilioni
Wabunge hao wamemtaka CAG kufanya ukaguzi maalumu wa fedha hizo na deni la Taifa huku wakisema kama Dk. Mpango ameshindwa kuongoza wizara hiyo ni bora akajiuzulu ili asiwe waziri wa fedheha.
Hoja hiyo imeibua mvutano bungeni kati ya wabunge hao, Waziri Mpango na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiwazuia kujadili ripoti hiyo ndani ya Bunge.
Akianza kuchangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya wizara ya fedha na mipango ya mwaka 2018/19, Mnyika amesema waziri wa fedha, Dk Mpango na taasisi zilizo chini yake, zinaandika barua kwamba mtu fulani asipewe msahama wa kodi halafu mlango wa nyuma anakwenda kutoa msamaha, kama sio fedheha ni nini?
Kauli hiyo ilimnyanyua, Dk Mpango ambaye alisema; “Mheshimiwa Mwenyekiti (wa Bunge- Najima Giga) naomba (Mnyika) athibitishe hilo.”
Mnyika akiendelea kuchangia amesema kumekuwa na kawaida wizara ya fedha kutoa kauli humu bungeni zinazokinzana.
“Aprili 20, 2018 Naibu waziri wa fedha (Dk Ashatu Kijaji) alitoa kauli humu bungeni kuhusu utata wa Sh. 1.5 trilioni ambazo hazijulikanani zimeenda wapi. Akasema Sh. 209 bilioni zimepelekwa Zanzibar, nimefuatilia mjadala wa baraza la wawakilishi sijaona hilo, CAG achunguze na ufanyike ukaguzi maalum,” amesema Mnyika.
Baada ya kutoa kauli hiyo, Waziri Mhagama amesimama na kusema; “Kauli za mawaziri, huwa hazijadiliwi bungeni, ninaomba nisisitize kauli za mawaziri hazijadiliwi bungeni.”
Waziri Mhagama amesema ripoti za CAG zitajadiliwa ndani ya Bunge mara baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuijadili na kuwasilisha taarifa yake ndani ya Bunge.
“Kwa hiyo hapa ndani ya Bunge tutaenda na kanuni na kama ni kujadili nje ya bunge wako wabunge wengine watalijadili,”amesema.
Baada ya kumaliza, kelele ziliibuka kutoka upinzani wakipinga huku Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga akimtaka Mnyika kuendelea kuchangia.
“Lazima CAG akalifanyie uchunguzi maalumu suala la Sh 1.5trilioni na kuhusu vile vifungu namba 22 kuhusu deni la Taifa,”amesema Mnyika
Kwa upande wake, Mdee amesema taarifa ya CAG ni halali kwa wabunge kulijadili.
Mdee amesema Waziri Mpango anatakiwa ajibu hoja kuhusu Sh. 1.5 trilioni na Sh. 200 bilioni zilizotajwa kupelekwa Zanzibar ni zipi?
Hata hivyo, Spika Job Ndugai alimtaka Mnyika kujiandaa kuthibitisha hoja yake kuhusu Dk. Mpango kuzuia msamaha wa kodi.