- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: GARI ZA SEREKALI ZINAZOVUNJA SHERIA KUCHUKULIWA HATUA
Dar es Salaam: Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limepiga marufuku magari yote ya serikali, magari ya vyombo vya ulinzi na usalama na yale ya wagonjwa kupita kwenye barabara zisizo ruhusiwa kwa sababu sio matumizi sahihi.
Akitoa kauli hiyo leo June 14 Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mabosasa ikiwa ni siku tatu baada ya gari la wagonjwa la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuligonga lori na kusababisha vifo vya watu wanne wakiwamo wanafunzi wawili wa chuo hicho.
Amesema wanaoongoza kuvunja sheria ni magari ya serikali ambayo hupita barabara za magari yaendayo kasi na zile zilizokatazwa kupita. "Barabara imetengwa kwa ajili ya magari yaendayo kasi matokeo yake wanaleta vurugu na wengine kusababisha ajali" amesema Mambosasa. Amesema jeshi hilo litaendesha msako mkali na yeyote atakayekamatwa, sheria itafuata mkondo wake.