Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 7:39 pm

NEWS: FAMILIA YA HECHE YAKATAA FIDIA YA SEREKALI KWA MWANAO ALIEFARIKI

Tarime: Msemaji wa familia ya marehemu Sunguta heche , Wegesa Suguta alisema hawatapokea fidia kutoka kwa mtu au taasisi yoyote na hawatalipiza kisasi dhidi ya yeyote akiwemo askari anayetuhumiwa kuhusika na kifo cha ndugu yao. Kauli hiyo pia iliungwa mkono na mbunge Heche aliyeenda mbali kwa kuitaka polisi kote nchini kuhakikisha matukio ya aina hiyo hayatokei kwa raia anayekuwa mikononi mwao.

“Lazima raia wawe na amani na salama wanapokuwa mikononi mwa polisi kwa tuhuma yoyote,” alisema. Kwa upande wake, Kiboye aliueleza umati wakati akitoa salamu za pole kuwa yeye alifika kwenye msiba huo kama rafiki na sehemu ya familia na ukoo wa Suguta. Pia alitumia fursa hiyo kulaani mauaji ya kijana huyo na kuwataka polisi kuzingatia weledi na sheria ili kuepuka matukio ya aina hiyo. Askari polisi William Marwa amekwishafikishwa mahakamani akikabiliwa na shtaka la mauaji akidaiwa kumuua Chacha kwa kisu usiku wa Aprili 27

Chacha Suguta (27), ndugu wa Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche aliyefariki dunia akidaiwa kuchomwa kisu akiwa mikononi mwa polisi, alizikwa jana nyumbani kwao katika Kijiji cha Nyabitocho wilayani humo. Ingawa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima aliyefika nyumbani kwa marehemu kuhani msiba aliahidi kuwa Serikali itashirikiana na familia katika msiba huo, hakuna kiongozi yeyote wa Serikali wala Jeshi la Polisi ngazi ya mkoa na wilaya aliyehudhuria mazishi.

Samuel Kiboye ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa mara ndie kiongozi pekee wa chama hicho kuhudhuria mazishi hayo.