- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ESTHER MATICO APANIA KUGOMBEA USPIKA 2020
Mbunge wa Tarime Mjini (Chadema) Esther Matico amepania kugombea kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania iwapo chama chake kitashika Hatamu mwaka 2020.
"Mwaka 2020 nadhani nitagombea nafasi hiyo ya Spika nakiombea chama changu kishinde na kuongoza serikali.
Akiongea na kituo cha EATV kupitia KIKAANGONI Matico amesema "Nikiwa Spika nitasimamia misingi na utaratibu pamoja na kusimamia nini kazi ya bunge. Kazi ya bunge mojawapo ni kusimamia na kuishauri serikali hivyo kama ni mbunge wa chama changu au hata wa upinzani akisimama kuisimamia vyema na kuishauri serikali ningemuacha aongee, ndiyo kazi ya bunge na hiyo ndiyo njia ya kuishauri serikali pale ambapo inaenda kinyume na mambo yanayotarajiwa," alisema Matiko.
Matiko ameongeza "Ningekuwa nawaambia ukweli kabisa hata kwenye vikao vya chama kwamba mimi ni spika na bunge ni muhimili unaojitegemea katika kutunga sheria na serikali ni muhimili mwingine hivyo chama changu itabidi kinisamehe kwa hilo. Ningekuwa spika wa mfano. Ningewashauri kwamba ikipitishwa bajeti wakaitekeleze siyo bunge linapitisha bajeti hii serikali inatekeleza vingine wakati mimi ni spika".