- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Donald Trump atoa mshahara wake sadaka kwenye mashirika ya kijamii
Washington: Katika Dunia kuna mambo mengi ya kushangaza, sasa Rais wa Marekani Bw Donald Trump ameshangaza wengi baada ya kutoa taarifa kupitia Msemaji wa ikulu ya White House Bw Sean Spicer amesema Rais Donald Trump atatoa mshahara wake kama hisani kwa mashirika yanayosaidia wasiojiweza katika jamii.
Sean Spicer amesema anataka waadhishi wa habari wanaoripoti taarifa kuhusu White House na Rais wa Marekani wamsaidie kuchagua nani wanafaa kupewa pesa hizo.
Mshahara wa Bw Trump utakuwa umefikia dola 400,000 kufikia mwisho wa mwaka.
Wakati wa kampeni za urais, Bw Trump alisema kwamba hakupanga kupokea mshahara wake na kwamba badala yake angepokea dola moja pekee ambayo ni lazima kisheria.
Alikosolewa wakati wa kampeni baada ya taarifa kuibuka kwamba alikuwa ametoa kiwango kidogo sana cha pesa kama hisani licha ya utajiri wake mkubwa.
viongozi walio wahi kufanya Hivyo
Bw Trump si kiongozi wa kwanza wa Marekani kukataa mshahara.
Herbert Hoover, aliyekuwa ametajirika kupitia biashara ya madini kabla ya kuingia madarakani, na John F Kennedy, aliyerithi utajiri mwingi, wote walikataa kupokea mashahara na badala yake wakatoa pesa hizo zisaidie wasiojiweza katika jamii.
Meya wa zamani Michael Bloomberg, gavana wa zamani wa California Arnold Schwarzenegger na gavana wa zamani wa Massachusetts Mitt Romney pia walikataa kupokea mishahara yao.
Mark Zuckerberg, mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, ndiye mfanyakazi anayelipwa mshahara wa chini zaidi katika kampuni hiyo.
Aidha, ni miongoni wa CEO (Afisa Mkuu Mtendaji) wengi ambao hulipwa mshahara wa $1 pekee.
Sergey Brin na Larry Page wa Google pia wamekuwa wakilipwa $1 kwa mwongo mmoja sasa.