- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DODOMA WAANZA KUPATIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA
Jijini Dodoma zoezi la uwandikishaji limeendelea sambamba na Ugawaji Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi ambao tayari wamekamilisha hatua zote za usajili.
Kwasasa Ugawaji Vitambulisho vya Taifa unafanyika katika Ofisi za Watendaji wa Mitaa na kwenye Ofisi ya Wilaya ya Dodoma iliyoko ghorofa namba 5 Jengo la Hazina.
Akielezea mafanikio hayo Afisa Usajili wa Wilaya ya Dodoma Ndg Khalid Mrisho amesema Wilaya yake imejipanga katika kuhakikisha kukamilika kwa Usajili kunakwenda sambamba na kasi ya Uzalishaji ili kuwawezesha wananchi kupata vitambulisho vyao kwa wakati badala ya kusubiri kwa muda mrefu.
“ Ugawaji wa Vitambulisho kwa sasa umerahisishwa tofauti na zamani ambapo mtu ilikuwa lazima kufika ofisi zetu kuchukua Kitambulisho; kwa sasa kutokana na usajili unaoendelea kwenye mitaa na vijiji vitambulisho vikishazalishwa wananchi wanapelekewa huko huko walipo kupitia watendaji wa Mitaa na Vijiji wanakoishi kuwagawia kama inavyoendelea sasa kwenye baadhi ya mitaa” alisisitiza.
Amesema ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa unaofanyika sasa kwenye ofisi ya Wilaya ni kwa wale watumishi wa Umma tu ambao kwa sababu mbalimbali walishindwa kufika kuchukua Vitambulisho vyao sambamba na kufanya usajili kwa watumishi wapya ambao hapo awalli hawakusajiliwa. Ila kwa wananchi vitambulisho wanachukulia kwenye mitaa na vijiji waliko.
Sambamba za zoezi la Usajili na Ugawaji Vitambulisho linaloendelea mkoani humo Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeanza maandalizi ya zoezi la Usajili wa Machinga maarufu kama Watarazaki, zoezi ambalo limelenga kuwapatia vitambulisho vitakavyowawezesha kufanya shughuli zao za kibiashara bila kubughudhiwa.
Baadhi ya mikoa tayari wameanza usajili wa Wamachinga maarufu Watarazaki ambao zoezi hilo linalenga kuwapata vitambulisho vya biashara ambavyo utambuzi wake unategemea Utambulisho wa Taifa.