- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CUF TIMU LIPUMBA WAPITISHA 49 KUGOMBEA UCHAGUZI WA MARUDIO
Dar es Salaam: Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Profesa Ibrahim Lipumba anayetambulika na msajili wa vyama vya siasa kimetangaza kushiriki uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani katika kata 79, ambapo wanachama 49 wamepitishwa na chama hicho kuwania udiwani katika kata hizo.
Akizungumza Leo July 9 mkurugenzi wa habari na uhusiano kwa umma wa chama hicho, Abdul Kambaya amesema mwitikio umekuwa mzuri, wanachama wengi wana shauku ya kushiriki uchaguzi huo.
Juzi CUF upande wa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Lipumba anayetambulika na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, walitangaza kushiriki uchaguzi katika kata hizo na jimbo la Buyungu.
Kambaya amesema tayari CUF wameanza mchakato wa kumsaka mgombea wa ubunge katika jimbo la Buyungu.
"Mambo yanakwenda vizuri na kwa kasi tayari wabunge wetu wapo kule Kakonko kumtafuta mtu mwenye sifa ya kukiwakilisha chama jimbo la Buyungu, itakuwa hivyo pia Jang’ombe watapatikana watu sahihi,"amesema.
Kuhusu kushirikiana na vyama vingine vya upinzani kama ilivyofungua milango chama cha ACT-Wazalendo, Kambaya amesema CUF haina mpango huo.
"Sisi tumeingia moja kwa moja hatuna mpango wa kushirikiana, tunasimamisha wagombea wetu, wao kama wanataka kupata uzoefu waendelee,” amesema Kambaya.
"Huo mchezo tuliufanya mwaka 2015 na tumeona madhara yake, jimbo la Segerea lilikuwa la CUF lakini kilichotokea wote tuliona.”