Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 11:10 pm

NEWS: CHAMA CHA WAFUGAJI WATISHIWA KUPELEKWA POLISI KISA MCHANGO WA MADAWATI.

Dodoma: Chama cha wafugaji ambacho hakijasajiliwa kisheria kijiji cha Mpamantwa wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wanatishiwa kupelekwa polisi na viongozi wa serikali ya mtaa kwa kile kinachodaiwa kuahidi kununua madawati 30 kwa ajili ya kusaidia watoto wao wanaosoma mashuleni.

Katibu wa chama cha wafugaji Mussa amesema utaratibu wa uchangiaji wa madawati ulikuwa kwa kila kitongoji na makubaliano ilikuwa kwa kila ng'ombe 1 atalipiwa TSH. elfu 1000 kama unang'ombe mia 200 Utalipa tsh laki mbili [ 2] nakuona utaratibu huo unawanyonya wafugaji kama wafugaji wakaamuwa kuanzisha chama chao ili waweze kusaidiana wasiweze kuwakandamiza wengine ndipo wakaanzisha chama na kuahidi wafugaji wote watanunua madawati 30.

Mussa ameongeza kuwa baada ya kuahidi madawati hayo ufuatiliaji wa viongozi wa chama ukawa hafifu ndipo baadhi ya wanachama wakaamuwa kujiondoa na uwanachama kabla ya ile ahadi ya ununuzi wa madawati haujatekelezewa ndipo uongozi wa mtaa ukaanza kumtishia katibu kuwa kama wafungaji hawataweza kulipa yeye atawajibika kununua madawati yote kama atashindwa hatua za kisheria zitachukuliwa zidi yake ikiwemo kupelekwa polisi.

Naye Mwenyekiti wa kijiji Bosco Emanuel amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa kwanza swala la uchangishaji wa madawati ni la hiyali ya mtu hakuna mtu anayelazimishwa na hakuna mtu atakaye pelekwa polisi ila katika swala la uhamasishaji labda kauli wanazotumia watu wengi wanashindwa kuwaelewa.

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Bahi Elizabeth Kitundu amesema ni kweli mchango huo upo ila swala la kumpeleka mtu polisi kwa ajili ya mchango wa madawati ni kikosa kwanza sera ya mchango wa madawati ni hiyali ya mtu atoe au asitoe wala si lazima. pia ameongeza kuwa anawaomba wananchi watoe kwani ni kwaajili ya manufaa ya watoto wao na maendeleo ya kijiji chao.