- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CAG ALALAMIKA KUPEWA BAJETI NDOGO KWENYE SEKTA YAKE
Dodoma: Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Profesa Mussa Juma Assad amesema ofisi yake imefanikiwa kutoa taarifa kwa wakati, kila inapofika Machi 30 ya kila mwaka licha ya kukabiliwa na ufinyu wa bajeti katika Sekta hiyo anayoiongoza.
Profesa Mussa Juma Assad
Profesa Assad ameyasema hayo Jana Mei 14 jijini Dodoma kwenye mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, ambao unalenga kupitisha bajeti ya mwaka na kujadili masuala ya kiutendaji ambayo yanawasilishwa na kuitishwa na wajumbe.
Akizungumza katika mkutano huo, CAG amesema ufinyu huo unaosababisha shughuli za kiofisi kutofanyika pamoja na kushindwa kutekeleza majukumu ya dharula yanayoibuka nje ya ukomo wao wa bajeti.“Baraza hii limekuwa na ufanisi mkubwa katika kusimamia majukumu yake kama yalivyoainishwa kwenye mkataba,”amesema Prof. Assad Amesema pamoja na mafanikio mbalimbali ambayo ofisi hiyo imeyapata, bado zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili na zinahitaji utatuzi wa kina.Amezitaja changamoto nyingine kuwa ni kushindwa kukamilisha ujenzi kwa ajili ya Ofisi katika mikoa iliyolengwa kutokana na kutotolewa kwa fedha za maendeleo kama ilivyopangwa na kwa wakati.
Aidha amesema katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa Fedha 2017/18 hadi kufikia Machi, 2018 Ofisi ilishindwa kuwajengea uwezo watumishi kulingana na viwango vya kimataifa vya ukaguzi kutokana na ufinyu wa bajeti.“Kuna changamoto ya mwenendo wa upatikanaji wa fedha za matumizi mengineyo na maendeleo kutoka mfumo mkuu wa serikali kutoendana na mahitaji halisi ya majukumu ya Taasisi hususani ukaguzi na mafunzo kwa watumishi,”amesema.
Wajumbe wa mkutano huo
Pia kwa upande wake Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais ,Utumishi, Dk.Laurean Ndumbaro ameitaka ofisi ya Taifa ya ukaguzi kutekeleza agizo la serikali kuhamishia shughuli zake mkoani Dodoma.Dk. Ndumbaro amesema tayari viongozi mbalimbali wa serikali walishahamia, hivyo ni mategemeo yake kuwa Ofisi ya Taifa ya ukaguzi nayo pia ipo katika mkakati wa kuhamishia shughuli zake jijini Dodoma kama ambavyo taasisi nyingine zimefanya. Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais ,Utumishi, Dk.Laurean Ndumbaro