Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 3:28 pm

NEWS: BWAWA LA UMEME LABOMOKA NA KUANGAMIZA WATU 24 NCHINI KENYA

NAIROBI: Idadi kubwa ya Watu wamepoteza maisha baada ya bwawa la kufulia umeme kubomoka katika mji wa Solai, karibu kilomita 200 kaskazini-magharibi mwa Nairobi nchini Kenya, afisa wa serikali amesema leo Alhamisi. Taarifa za awali zinaripoti kuwa Takribani watu 24 wamefariki na wengine 2,500 kukosa makazi baada ya bwawa hilo kubomoka.


Gavana wa mkoa wa Nakuru amedhibitishatukio hilo na kiwango cha uharibifu kinaendelea kutathminiwa na shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limetangaza kwenye Twitter kwamba limewaokoa watu 39.

Kupasuka kwa bwawa hili kumesababishwa na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha mashariki mwa Afrika kwa miezi miwili sasa.

Tangu mwezi Machi, mvua hizo zimeua watu 132 na kusababisha zaidi ya watu 220,000 kuyahama makazi yao katika kaunti 32, serikali ya Kenya imesema.