- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News; Bunge la Uingereza Kujiondoa Jumuiya ya Ulaya
Uingereza; Bunge la Uingereza limetoa idhini ya mwisho ya sheria muhimu katika hatua ya mchakato wa kuelekea kutaka kujitoa katika jumuiya ya Ulaya.
Serikali ya Uingereza inapanga kuanza hatua rasmi za kujiondoa ndani ya jumuiya ya Ulaya ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.
Hatua hii inatarajiwa kuwa na utata kufuatia tangazo la Scotland linalodai kuwa wanampango pia wa kuwa na kura ya maoni kuhusiana na kujitenga kwao na Uingereza na kisha kuwa taifa huru.
Aidha Waziri mkuu kwa mjibu wa kifungu namba 50 kinampa uwezo kuitisha mchakato huo mapema zaidi kuanzia siku ya leo jumanne.
Hata hivyo taarifa kutoka ndani ya bunge la Uingereza zinasema kuwa hakuna uwezekano wa mchakato huo kuanza wiki hii na kwamba Waziri mkuu atatakiwa kusubiri hadi mwisho wa mwezi huu muda ambao ni rasmi.
Chama upinzani cha Liberal kimesema kuwa serikali imeshindwa kuonyesha msimamo juu ya haki za raia wa EU wanaoishi nchini Uingereza na kutoa wito kwa makundi mbali mbali kusisitiza juu ya mabadiliko.