- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : BOTSWANA WAMVAA TRUMP KUFUATIA KUZITUSI NCHI ZA AFRIKA
BOTSWANA WAMVAA TRUMP KWA ‘KUZITUSI’ NCHI ZA AFRIKA
SERIKALI ya Botswana imemshutumu Rais wa Marekani, Donald John trump kwa matamshi yake kuwa Mataifa ya Afrika ni “machafu” na kusema tamko la rais huyo ni la kukosa kuwajibika, la kukera na “ubaguzi wa rangi”. Trump alisema hayo alipokuwa akizungumzia Sera ya Uhamiaji ya Marekani, ambapo alisema anafikiri watu kutoka Haiti, El Salvador na nchi za Afrika hawafai kuruhusiwa kuingia kama wahamiaji Marekani.
Kupitia taarifa maalum, Botswana imemwita Balozi wa Marekani nchini humo kufafanua iwapo Marekani inachukulia taifa hilo la Kusini mwa Afrika kama “taifa chafu” na taifa la mabwege huku ikieleza tamko la Trump ni kukosea heshima taifa ambalo lina urafiki na uhusiano wa kibalozi.
Aidha Botswana imeitaka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC pamoja na Umoja wa Afrika kushutumu tamko hilo la Trump ambaye kwa upande wake amejitetea na kusema hakutumia maneno hayo, lakini akasema aliyoyasema yalikuwa na “lugha kali