- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Boss wa Madawa ya kulevya Duniani “El Chapo” awasili chini marekani
New York: MFALME wa madawa ya kulevya Duniani Joaquin “El Chapo” Guzman, ambaye amejipatia sifa kubwa nchini Mexico baada ya kutoroka jela na miaka kadhaa ya kuwa juu ya sheria, amewasili jijini New York, Marekani
Guzman atafikishwa mahakamani huko Brooklyn, ambapo atashitakiwa siku za baadae. Hali ya usalama imaimarishwa katika jela anayoshikiliwa huko Manhattan, chanzo ndani ya vyombo vya usalama kimesema. Daraja maarufu la Brooklyn litafungwa wakati mhalifu huyo akipelekwa mahakamani.
Kumsafirisha Guzman kwenda Marekani ni kama kulipangwa kufanyika wakati huu. Mamlaka nchini Mexico walitaka kumkabidhi Guzman, mkuu wa kundi la Sinaloa, kabla ya kuapishwa kwa Rais Mteule Donald Trump, afisa mmoja wa Marekani aliliambia shirika la habari la CNN. Trump aliiudhi Mexico wakati wa kampeni zake kwa kuitaka ilipie ukuta utakaozitenganisha nchi hizo mbili.
Guzman na viongozi wengine wa makundi ya kihalifu waliitwa mahakamani katika mahakama huko Brooklyn Marekani kwa mashtaka ya kushiriki katika kuingiza kiasi cha paundi 264,000 za cocaine nchini Marekani kati ya mwaka 1990 na 2005.
Guzman pia anakabiliwa na mashtaka huko California, Texas, Illinois, Florida na New Hampshire. WIzara ya Mambo ya Nje ya Mexico imesema kuwa imepewa uhakika kwamba iwapo Guzman atakutwa na hatia, hatokabiliwa na adhabu ya kifo. Mexico inapinga adhabu ya aina hiyo.
Mashtaka nchini Marekani yanaeleza kuwa kundi la Sinaloa hutumia mauaji, utekaji nyara na hongo katika shughuli zake.
Kwa miaka kadhaa, amejizolea sifa nchini mwake, hadi kufikia kuimbiwa wimbo unaoitwa “narcorridos,” wimbo mahsusi kwa ajili ya makundi hayo ya kusafirisha madawa ya kulevya.
Usafirishaji wa heroin, bangi, cocaine na methamphetamine, aina ya madawa ambayo hutengenezwa maabara, kuelekea nchini Marekani kutoka Mexico itaendelea. Biashara hiyo inakadiriwa kuwa na thamani ya dola kati ya bilioni 19 hadi 20 kwa mwaka, kulingana na taarifa ya usalama ya Wizara ya Ndani ya Marekani, DoH.
Kundi la Sinaloa chini ya Guzman limekuwa linamiliki sehemu kubwa ya biashara hiyo, kutokana na mikakati tata ya kibiashara ya Guzman na umiliki wa njia za usafirishaji ambao ni wa Sinaloa.