Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 11:45 am

NEWS: BOLISA YALIA KUKATIKA MAWASILIANO YA BARABARA.

KONDOA: Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini katika Halmashauri ya Mji wa Kondoa mkoani Dodoma (Tarura) wametakiwa kutengeneza mifereji pembezoni mwa barabara zilizofanyiwa matengenezo ili ziweze kupitika muda wote.

Hayo yalisemwa na diwani wa kata ya Bolisa Abed Boki alipokuwa akizungumzi hali ya barabara ya kuelekea Bolisa kutoka Kondoa Mjini kwa kipindi cha mvua zinazoendelea kunyesha Kondoa Mjini.

Alisema kuwa barabara iliyotengenezwa imeanza kuweka mashimo makubwa pembezoni kutokana na kukosekana kwa mifereji ya kupitisha maji hali inayotishia kukatika kwa mawasilianao.

“barabara hiyo kutokana na mashimo hayo ambayo yanaweza kupelekea kukatika kwa barabara hiyo na kukosekana kwa mawasiliano kati ya Bolisa na Gubali”alisema.

Aidha aliongeza kuwa mashimo hayo yapo katika kijiji cha Itiso, Poisi na Bolisa hivyo Tarura, iende kufanya utafiti mapema kabla ya mvua kubwa zaidi kunyesha na kuleta madhara kwani kutokana na mvua za sasa hali ya usafiri pia imeanza kuleta shida.

Akielezea changamoto hiyo Kaimu Meneja wa TARURA Kondoa Mji Bwana Wera Kweka alisema kwasasa barabara hiyo bado ipo chini ya mkandarasi (MISPA CONSTRUCTION) ambao wanaendelea na matengenezo na moja ya kazi katika mkataba ni kuweka makalvati na kufungua mifereji ili maji yawe na mwelekeo na kuepusha uharibifu.

Hatahivyo aliongeza kuwa kwasasa hali ni mabya zaidi katika maeneo ya Serya kwenda Mongoroma ambapo mawasiliano katika vijiji hivyo yamekatika na kuwaagiza wakandarasi waliopo katika maeneo hayo kujenga barabara hiyo haraka na kuhakikisha inapitika kipindi chote.