Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 6:53 pm

News: Babu wa Loliondo ahidi kurudi tena kwenye TIBA

ARUSHA: Nikisema kikombe cha babu mawazo yanakujia kuwa ni yule Babu wa Samunge au Loliondo anaitwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile, huyu babu bado yupo na shughuli zake za kutoa kikombe cha dawa anayodai inatibu magonjwa yote yanayomkabili binadamu.

Hata hivyo, baada ya ukimya wa muda mrefu babu ameibuka na kuitaka kwa mara nyingine Serikali kuboresha miundombinu ya Loliondo kwa kuwa kuna mambo makubwa yanakuja kutokana na maono anayoonyeshwa. Akizungumza nyumbani kwake katika Kijiji cha Samunge,

Tarafa ya Sale jana, Mchungaji Mwasapile alisema watu waliokuwa wanakwenda kwa wingi miaka iliyopita wamepungua sana na sababu ni kuwa idadi kubwa ya walipokea uponyaji wakati huo.
Mchungaji huyo mstaafu alisema wito anaoutoa kwa Serikali kuboresha miundombinu unatokana na mambo makubwa anayoonyeshwa yatakayokuja wakati ambao Mungu ameupanga.