Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 3:40 pm

NEWS: ASILIMIA 70 KIGOMA HAMNA WATUMISHI WA AFYA.

Mkoa wa kigoma unakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi katika kada ya afya kwa asilimia 70 hali ambayo inasababishwa na watumishi wengi wanaopangiwa maeneo ya mkoa wa Kigoma kuhama siku chache baada ya kuripoti kazini wengine wakishindwa kuripoti kutokana na jiographia ya mkoa huo.

Jiographia ya mkoa huo inaelezwa kuwa ni kikwazo cha watumishi wengi kutoka nje ya mkoa huo kufanya kazi wanazopangiwa ndani ya mkoa hali ambayo inasababisha kuwa na upungufu mkubwa wa watumishi.

Mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma Dr. Paul Chaota amesema kuwa katika sekta ya afya mkoa unakabiliwa na upungufu wa watumishi kwa asilimia sabini.

Pamoja na utatuzi wa changamoto zingine katika sekta ya afya ikiwemo ya watumishi,serikali katika kuhakikisha huduma ya afya ya mama na mtoto inaboreshwa zaidi na kudai kuwa huduma hiyo ndiyo kipaumbele.