Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 5:31 pm

NEWS: AMLAWITI MTOTO WA MWAKA MMOJA ILI KUPATA MALI

TABORA: Mkazi mmoja aliyefahamika kwa jina la Kadege Thabit (18), mkazi wa Utemini wilaya ya Uyui mkoani Tabora anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa mwaka mmoja na miezi miwili kutokana na imani za kishirikina . Kadege aliahidiwa na mganga wake kumuingilia kinyume na maumbile mtoto wa mwaka mmoja ili kuweza kupa mali nyingi kutoka kwa mganga huyo.

Tukio hilo, limetokea Juni 21 saa tatu asubuhi katika kata ya Ndono Mkoani humo.

Akizungumzia tukio hilo leo Juni 27, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa, amesema mtuhumiwa alimchukua mtoto huyo na kumwingilia kinyume cha maumbile. Kamanda Mutafungwa ameeleza kwamba mtuhumiwa alitenda tendo hilo baada ya kumchukua mtoto huyo kutoka kwa mama yake akidai anaenda kumnunulia maandazi.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa baada ya kumnunulia maandazi mtoto huyo alimpeleka chumbani kwake akafunga mlango ndipo akatenda unyama huo. “Uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la polisi umebaini kuwa sababu za kufanya ukatili huo ni imani za kishirikina, na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio hilo bado unafanyika,” amesema Kamanda Mutafungwa amefafanua kwamba mtuhumiwa baada ya kukamatwa na kuhojiwa alidai kuwa alitenda kosa hilo kutokana na maelekezo ya mganga mmoja wa kienyeji kwamba ataweza kupata mali nyingi