- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : ALIYEKUWA MGOMBEA URAIS NCHINI KONGO ATUPWA JELA MIAKA 20
Aliyekuwa mgombea wa urais wa chama cha upinzani cha FROCAD nchini Jamhuri ya Kongo Brazaville, Jenerali mstaafu Mokoko amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kuhujumu usalama wa taifa na kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Waendesha mashtaka katika kesi hiyo wamesema Mokoko na watuhumiwa wenzake kadhaa wamepatikana na hatia ya kukusanya silaha kinyume cha sheria mwaka 2005, kwa lengo la kuipindua serikali.
Mokoko ambaye aligombea urais katika uchaguzi uliofanyika mapema mwaka 2016, alitiwa nguvuni na vyombo vya usalama mwezi Juni mwaka huo.
Serikali ya Rais Denis Sassou Nguesso imekuwa ikimtuhumu jenerali huyo mstaafu ambaye alikuwa mpatanishi katika mchakato wa mgawanyo wa madaraka wakati wa vita vya ndani vilivyotokea nchini humo katika muongo wa 1990, kuhusika na jaribio la mapinduzi ya kijeshi la mwaka 2007.
Jenerali mstaafu Mokoko amekuwa kimya tangu kesi dhidi yake ianze Jumatatu iliyopita, huku waendesha mashitaka wakisema kuwa kunyamaza huko kunaashiria kuwa mwanasiasa huyo mkongwe wa nchi hiyo ana hatia.
Philippe Esseau, wakili wa Mokoko amesema, "Haki haijafanyika, Jean-Marie Michel Mokoko hapaswi kushitakiwa kwa kuwa ana kinga, amezuiliwa kinyume cha sheria na uamuzi huo hauna thamani."
Mokoko alitunukiwa tuzo ya heshima ya Commander of the Congolese Order of Merit na kwa msingi huo wakili wake anasema hakupaswa kukamatwa, kushtakiwa wala kuhukumiwa.