Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 7:45 pm

NEWS: ALIYEJIFUNGUA MAPACHA AKIWA MAHABUSU AKOSA DHAMANA

Kilimanjaro: Mwanamke aliyejifungua watoto Mapacha akiwa Mahabusu ,Marry Lukumay ameendelea kusota Gerezani na watoto wake baada ya kukosekana kwa wadhamini wenye sifa zinazokidhi masharti yaliyotolewa na Mahakama.

Moja ya masharti ya dhamana yake yaliyotolewa na Mahakama ya Hakimu mkazi ,Moshi ni pamoja na kuwa na wadhamini wawili ambao ni wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro watakaosaini Fungu la Dhamana la kiasi cha sh laki tano kila mmoja.Marry Lukumay mkazi wa Babati mkoani Manyara kwa mara nyingine alifikishwa mahakama ya hakimu Mkazi ,Moshi baada ya kukamatwa Oktoba 15 mwaka jana kwa madai ya kukutwa na Mirungi kilogramu 10 mkoani humo.

Katika shauri hilo namba 182 la mwaka 2017 ,mwendesha mashtaka upande wa Jamhuri ,Lilian Kowelo aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kwa shauri hilo kutokana na upelelezi kutokamilika .Hakimu anayesikiliza shauri hilo ,Pamela Meena alikubaliana na ombi hilo na kupanga June 27 mwaka huu ,mtuhumiwa kufikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa kwa shauri hilo.

Mary anayeshikiliwa katika Gereza la Karanga mkoani Kilimanjaro alisema wakati anakamatwa tayari alikuwa na ujauzito wa miezi miwili na Aprily 8 mwaka huu alijifungua watoto hao Mapacha katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro