- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AHUKUMIWA MIAKA 3 JELA KWA KOSA LA KUMTUKANA DC
TABORA: Mahakama ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, imemhukumu mkazi wa mtaa wa barabara ya Mbutu, Mohamed Ahmed (54) kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kutiwa hatiani kwa kumtishia na kumtolea lugha ya matusi Mkuu wa Wiilaya hiyo, John Mwaipopo.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Elimajidi Kweyamba, alidai mahakamani hapo kwamba mshitakiwa, alitenda kosa hilo Januari 09, mwaka huu, saa 1:05 usiku katika maeneo ya barabara kuu ya lami ya Igunga mjini.
John Mwaipopo.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Igunga, Ajali Milanzi, Kweyamba amesema kuwa mshitakiwa huyo alimtolea Lugha ya matusi Kiongozi huyo wa Wilaya wakati akitekeleza majukumu ya agizo la upandaji miti kama lilivyotolewa maelekezo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassani.
Aidha, mwendesha mashtaka amedai kwamba katika kosa la pili, muda huo huo na tarehe hiyo hiyo, mshitakiwa akiwa na nia ovu, alimtishia maisha kwa maneno Mkuu wa Wilaya kuwa atamwonyesha na atahakikisha anahama Igunga kwa kumfanyia kitu kibaya.
Hata hivyo, baada ya kusomewa mashitaka yote mawili, mshtakiwa huyo alikiri kutenda makosa hayo.
Kabla ya kutoa hukumu, Hakimu Milanzi alisema kwa kuwa mshtakiwa amekiri mwenyewe makosa, atatumikia adhabu ya kifungo cha miaka mitatu gerezani, mwaka mmoja kwa kosa la kwanza na miwili kwa kosa la pili.