- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Adhabu zisizo stahili zamweka mwalimu matatani
Tanga.kutokana na miezi kadhaa iliyopita baada ya mwanafunzi Sebastian Chingulu wa form 3 wa shule ya sekondari mbeya day kudhibiwa na mwalimu Frank Msingwa hatimaye jeshi la Polisi Mkoani Tanga Linamshikilia mwalimu wa shule ya sekondari mkwakwani kwa kumpinga na kumsababishia madhara ya kiafya mwanafunzi Seleyman Mohamend miaka [18].
Mwanafunzi huyo alidaiwa kuchapwa viboko juzi asubuhi na mwalimu huyo wa zamu aliyekuwa akiwaadhibu wanafunzi waliochelewa na waliokuwa wakiiga kelele darasani .
Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba amesema tayari mwalimu huyo yuko mikononi mwa jeshi hilo kwa upelelezi wa suala hilo unaendelea.
Naye kwa upande wake , mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amewataka walimu kuwa waangalifu wakati wakuwadhibu wanafunzi ili kukwepa madhara kwa wanafunzi .
''Tunafuatilia kwa karibu tukio hilo hili Niseme kwamba kwamba tutachukua hatua stahiki ikithibitika kuwa umefanyika uzembe '',amesema Mwilapwa.
Baada ya kuchwapwa , mwanafunzi huyo amelazwa katika hospital ya Rufaa ya Bombo ikielezwa kwamba tayari amepata rufaa kuhamishiwa Hospital ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.