- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ACT WAZALENDO YAKOSOA MFUMO MPYA WA MKOPO KWA WANAFUNZI
Dar es salaam: Chama Cha ACT- Wazalendo kimeukosoa utaratibu mpya uliotangazwa na Bodi ya mikopo Tanzania (HESLB) kwa wanafunzi wa elimu ya juu ya mtoto ambaye mzazi wake anamiliki leseni ya biashara au Meneja wa taasisi yoyote inayotambulika atakosa mkopo, Chama hicho kimeishauri serikali kubadilisha mfumo kutoka katika mikopo na kuingia katika mfumo wa ufadhili.
.Akizungumza na wandishi wa habari jana Mei 13, 2018 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT, Likapo Likapo alisema kipengele hicho kitazalisha matabaka katika jamii kwa kuwatenga watoto wa wafanyabiashara.
“Kipengele hiki kinamaanisha kuwa mtu yeyote atakayesajili biashara yake Brela na TRA hata ya kunyoa tu mwanawe hatapata mkopo wa elimu juu jambo ambalo litazua hofu kwa wafanyabiashara,” alisema Likapo.
Alisema kipengele hicho kitawatia hofu wafanyabiashara kusajili biashara zao kwa hofu ya watoto wao kutokupata mkopo wa elimu ya juu.
“Hili litapunguza morali ya wafanyabiashara kulipa kodi kwa kuwa wakisajili biashara zao watatakiwa kuwalipia masomo ya juu watoto wao,” alisema Likapo.
Aliongeza kuwa hakuna sheria inayowataka wazazi wanaopeleka watoto wao katika shule binafsi kulazimika kusomesha bila ya kulipiwa mikopo ya elimu ya juu.
Aliongeza kuwa ni vema serikali ikafadhili masomo na malazi kwa wanafunzi na kama kuna mwanafunzi atahitaji fedha za kujikimu atalazimika kwenda kukopa katika taasisi za fedha.
Kauli ya ACT imekuja siku chache baada ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kutoa mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka 2018/19.
Katika mwongozo huo kuna kipengele kinachozuia kuomba mkopo wanafunzi ambao wazazi wao wanamiliki biashara au Meneja wa taasisi yoyote inayotambulika
Akizungumzia kuhusu kauli ya Rais Dk. John Magufuli kuhusu kufanya siasa vyuoni, Likapo alisema kauli hiyo itawaondolea vijana kujiamini na hivyo kuwa na kizazi cha watu waoga na wasiojiamini.