Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 1:30 pm

NEWS: ABURUZWA MAHAKAMANI KWA KUPIGA NA KUMCHOMA KWA PASI KIJANA MDOGO

Manyara: Mkazi mmoja wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, Bw. Nikodemu Johnson amefikishwa mahakamani kwa kosa la kumpiga na kumchoma kwa pasi ya umeme kijana mmoja mkazi wa Katesh wilayani humo.

Mshtakiwa alikana mashtaka hayo mbele ya Hakimu mkazi wa Wilaya Amani Petro Shao.

Ilidaiwa na mwendesha mashtaka kuwa Mei 28 mshtakiwa alimpiga na kumchoma kwa pasi ya umeme Christopher Bayanga (19) baada ya kumkuta kijana huyo kwenye nyumba ya mtuhumiwa.

Alidai kipigo alichomfanyia kijana huyo, hasa kuchomwa kwa pasi ya moto, kimemsababishia maumivu makali na kwamba maisha yake yalikuwa hatarini kwani alifungiwa ndani wakati huo.

Johnson yuko nje kwa dhamana hadi Julai 25 wakati kesi hiyo itakaposikilizwa.