Nchi hiyo kubwa barani Afrika imesubiri kusikia kama Kabila atagombea katika uchaguzi uliocheleweshwa kwa muda mrefu ukiwa umepangwa kufanyika mwezi Desemba licha ya muhula wake kikatiba kumalizika mwaka 2016. Rais Kabila amekataa kutangaza hadharani iwapo atagombea muhula mwingine madarakani au la, na wagombea urais wanatarajiwa kusajiliwa kati ya tarehe 25 mwezi huu hadi tarehe mosi Agosti.
Wiki iliyopita katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema alikubali kuahirisha ziara yake nchini Congo ili kumruhusu Kabila kutangaza maamuzi mazito. Kabila ambaye alichukua madaraka kutoka kwa baba yake aliyeuawa mwaka wa 2001, alimaliza muhula wake kisheria mwaka 2016 lakini vifungu vya katiba vilimruhusu kusalia madarakani hadi mrithi wake atakapopatikana.