- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NAPE: KWENYE CHAMA CHANGU CHA KIJANI NINAHISA NYINGI MENGINE BLANKA TU
Mbunge wa mtama kupitia CCM Nape Moses Nnauye amefunguka uwepo wa tetesi za Ubunge wake kuwa hatarini kutokana na kuwepo kwa taarifa za kupigwa chini wabunge 17 wa Mikoa ya kusini na Uwongozi wa juu wa chama cha mapinduzi CCM.
Akiongea Juzi na wananchi wa Mtama Nape alisema “Yapo maneno sasa, hatima ya mbunge wetu ni ipi? Tusipate shida. Kwenye chama changu cha kijani, nina hisa nyingi msipate shida,” alisema Nape.
“Najua mmenielewa, furaha yangu mimi ni kuwatumikia nyinyi, mengine yote blabla.”
Nape, ni mmoja wa wabunge takriban 17 kutoka mikoa ya Kusini waliopinga sheria hiyo inayoiruhusu Serikali kuchukua ushuru wote wa korosho inayouzwa nje badala ya kugawana na Mfuko wa Pembejeo kama ilivyokuwa awali, amesema mgogoro wa sheria hiyo iliyoligawanya Bunge, ulitokana na fedha hizo kuongezeka kutoka Sh800 milioni hadi kufikia Sh200 bilioni.
Nape alisema baada ya zao hilo kushuka, kiongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete aliamua kubeba mzigo huo kwa kuhakikisha madeni ya vyama vya ushirika yanabebwa na Serikali ili vikopesheke.
Alisema baadaye, wakulima na wadau wa korosho walikutana na kukubaliana kutoza ushuru kwa zao hilo litakapouzwa nje ili kusaidia maendeleo ya korosho na ndipo kukawa na ongezeko la zao hilo ambalo lilisababisha na bei kukua.
“Mwanzoni tulianza kwa Sh250, lakini mwaka jana tulifikia Sh4,000 kwa kilo,” alisema Nape na kubainisha kwamba hapo ndipo tatizo lilipoanza.