- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NANI HUFIKA KILELENI ZAIDI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME NA KWANINI
California: Tafiti nyingi zimekuwa zikifanyika kujua kama kuna ‘tofauti katika kufika kileleni,’ ambazo hutazama namna wanaume wanavyofika kileleni mara nyingi zaidi wakati wa kufanya mapenzi kuliko wanawake.Lakini ni kwa nini tofauti hii ya kijinsia ipo, na kitu gani kinaweza kufanyika ili kufikia kileleni kwa usawa?
Pamoja na yote, kiasi cha asilimia 60 ya wanawake wanakabiliwa na matatizo yanayotokana na masuala ya kujamiiana, yanayosababishwa na tatizo sugu la kushindwa kufika kileleni.
Wataalamu wanajibu baadhi ya maswali.
“Makundi yote ya wanaume – mashoga, wale wenye jinsia mbili, na wale wanaopenda watu wa jinsia tofauti – hufika kileleni kuliko makundi kama hayo ya wanawake,” alisema David Frederick, Profesa msaidizi wa saikolojia katika Chuo Kikuu cha Chapman nchini Marekani, ambaye amebobea katika masuala ya kujamiiana kwa binadamu.
“Makundi ya wanawake wanaolala na wanawake wenzao hufikia kileleni mara nyingi zaidi ya wanawake wanaolala na wanaume, japokuwa si mara nyingi kama wanaume,” alisema. “Kinachowafanya wanawake kufika kileleni ni suala kubwa ambalo wengi wamekuwa wanakisia tu. Kila mwezi, magazeti, majarida na hata makala za kwenye mitandao hutazama njia tofauti ambazo zinaweza kuwasaidia wanawake kufika kileleni kwa urahisi zaidi. Ni suala la uandishi wa vitabu kabisa. Kwa watu wengi, kufika kileleni ni sehemu muhimu katika mahusiano ya kimapenzi.”Kinachosababisha tafauti hiyo inaweza kuwa ni sababu ya kijamii au kutokana na mabadiliko ya kimaumbile kwa binadamu, Frederick alisema.
“Wanawake wanauwezekano mkubwa zaidi wa kushindwa kuridhika na hali fulani katika maisha yao kuliko wanaume, na na hilo huweza kuingilia maisha yao ya kingono. Hili linaweza kuathiri kuridhika kwao wakati wa kujamiiana na uwezo wa kufika kileleni iwapo watu wanakuwa wanapeleka nguvu zaidi katika mambo yanayowapa wasiwasi zaidi ya tendo lenyewe la ngono,” alisema.
“Lakini pia kuna unyanyapaa zaidi dhidi ya wanawake ambao wanakuwa wa kwanza kuomba ngono na wanaosema ni kitu gani wanapendelea kitandani,” alisema, na kuongeza, “kitu kimoja tunachofahamu ni kwamba kwa wapenzi wengi, kile wanachotamani wanashindwa kusema. Mpenzi mmoja anaweza kuwa anatamani kufanya mapenzi mara nyingi zaidi ya mwenzake. Katika mahusiano baina ya mwanaume na mwanamke, mtu huyo mara nyingi huwa ni mwanaume.”
Kwa hiyo, mwanamke anaweza kufanya mapenzi na mwenzi wake wakati mwingine akiwa hajisikii kufanya hivyo, na hivyo inakuwa ni vigumu zaidi kwake kufika kileleni, Frederick alisemaPia kuna wazo kwamba kufika kileleni kwa mwanaume kunasaidia kizazi, kwa kuwa uzazi unatokea iwapo mbegu zitatoka. Kwa wanawake, hata hivyo, hakuna uhusiano wa wazi baina ya kufika kileleni na uzazi, Frederick alisema.
“Lakini mamilioni ya miaka iliyopita, inaweza kuwa kulikuwa na uhusiano huo,” aliongeza.
“Nadharia mojawapo inasema kwamba kwa mababu zetu, kufika kileleni ilikuwa ni rahisi zaidi kwa sababu kazi yake ilikuwa ni kufanya yai la kike kutoka yaani ovulation. Hili hutokea kwa wanyama wengi,” alisema Frederick. “Mara moja kila mwenzi mzunguko wa hedhi ulianza kufanya kazi hiyo, hivyo kufika kileleni haikuhusishwa na uzazi kwa wanawake. Hili lilisababisha uwezo na wepesi wa kufika kileleni kwa wanawake kutofautiana kupitia mamilioni ya miaka na ndiyo maana kufika kileleni kwa wanawake kunatofautiana sana kwa wanawake kuliko ilivyo kwa wanaume.”
Baadhi ya wanawake wanaweza kuwa wameumbwa kufika kileleni mara nyingi, alisema Elisabeth Lloyd, profesa wa biolojia na filosofia wa Chuo Kikuu cha Indiana huko Bloomington, Marekani, ambaye ameandika kitabu juu ya sehemu za siri na kufika kileleni wakati wa kujamiiana.
Urefu baina ya kinembe na mlango wa mkojo kwa wanawake, ambapo mkojo hupita, inaweza kuongeza uwezekano wa mwanamke kufika kileleni, kulingana na utafiti, uliochapishwa katika jarida la Hormones and Behavior mwaka 2011.