Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 7:59 pm

NAKUSOGEZEA ORODHA YA MATAJIRI DUNIANI BILL GATE AONGOZA 2017

Washington: Uchumi wa matajiri Duniani umeendelea kuimarika kiasi ambacho umefanya idadi ya matajiri duniani kuongezeka kidogo Idadi ya mabilionea (wa dola) duniani imeongezeka kwa asilimia 13 na kufikia 2, 043.lakini kwa asilimia kubwa idadi yamatajiri imeendelea kubakia na sura ya majina yale yale tuliyo yazoea kuyaona kwenye sura ya watu wenye uchumi mkubwa Duniani, Mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates kwa mara nyingine anaongoza orodha ya jarida la Forbes ya watu tajiri zaidi duniani kwa mwaka huu.

matajiri

Kwa mujibu wa jarida hilo, mali ya Bw Gates imeongezeka hadi $86bn, kutoka $75bn.

Anafuatwa na Warren Buffett, aliyeongeza utajiri wake kwa $14.8bn hadi $75.6bn.

Rais wa Marekani Donald Trump, hata hivyoa meshuka nafasi 220 hadi 544 kwenye orodha hiyo ya matajiri na sasa ana mali ya $3.5bn pekee.

Forbes wamesema kushuka kwa utajiri wa Bw Trump kwa $1bn kulitokana na kuupungua kwa kasi ya sekta ya biashara ya ardhi na makao Marekani.

Katika orodha hiyo ya Forbes, mabilionea 183 walijipatia utajiri wao kupitia teknolojia, utajiri wao ukiwa jumla ya dola trilioni moja za Marekani.

Orodha hiyo imetawaliwa na mabilionea kutoka Marekani.

Wengine walio kwenye 10 matajiri zaidi ni mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos, ambaye amepanda hadi nambari tatu utajiri wake ukiongezeka kwa kiwango cha juu zaidi kuliko wa mtu mwingine yeyote duniani.

Utajiri wake uliongezeka kwa $27.6bn hadi $72.8bn.

Mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg yupo nafasi ya tano na mwanzilishi mwenza wa Oracle Larry Ellison alikuwa nambari saba.

Top 10 ya matajiri:

  • 1. Bill Gates (mwanzilishi mwenza wa Microsoft): $86bn
  • 2. Warren Buffett (mwekezaji Mmarekani): $75.6bn
  • 3. Jeff Bezos (mwanzilishi wa Amazon): $72.8bn
  • 4. Amancio Ortega (mwanzilishi wa Inditex): $71.3bn
  • 5. Mark Zuckerberg (mwanzilishi wa Facebook): $56bn
  • 6. Carlos Slim (mfanyabiashara kutoka Mexico): $54.5bn
  • 7. Larry Ellison (mwanilishi mwenza wa Oracle): $52.2bn
  • 8. Charles Koch (mfanyabiashara Mmarekani): $48.3bn
  • 9. David Koch (mfanyabiashara Mmarekani): $48.3bn
  • 10. Michael Bloomberg (mwanzilishi wa Bloomberg): $47.5bn