Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 8:25 pm

Mwakyembe "NIMARUFUKU KUFUNGA NDOA YOYOTE BILA CHETI CHA KUZALIWA"

Dar es salaam: Waziri wa katiba na sheria Dr. Harison Mwakyembe amepiga marufuku ya kufunga ndoa yoyote ile bila kuwa na cheti cha kuzaliwa amesema hayo akiwa katika ziara yake mkoani Morogoro na kuongeza kuwa serikali imeamua kufanya hivyo ili kupata takwimu sahihi za wananchi wake zitakazo saidia kupanga mipango ya kimaendeleo sambamba na kuzuia wageni kuingia kinyemela nchini. Mwakyembe amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za mwisho kwenye maswala ya Takwimu'


Pia amewataka Wakala wa Usajili wa vizazi na Vifo (RITA), kuhakikisha inasimamia sheria ya usajili ambapo amesema kuwa "bila kuwa na takwimu sahihi za vizazi na vifo ama ndoa inasababisha nchi kushindwa kusonga mbele kimaendeleo. “Wenzetu nchi zilizoendelea suala la usajili wamelipa kipaumbele lakini sisi bado tuko nyuma,

akatolea mfano pia kwa mkoa wa Morogoro kuwa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, inaonyesha kuna jumla ya wakazi milioni 2.2, lakini waliosajiliwa na kuwa na vyeti vya kuzaliwa ni asilimia 11 pekee huku wengine wakiwa bado hawasajiliwa,” alisema Mwakyembe. Pia aliwataka wanawake na wanaume wanaotaka kufunga ndoa wasikubali kuolewa wala kuoa mtu bila ya kuwa na cheti cha kuzaliwa aliyasema hayo akiwa kwenye ziara yake mkoani morogoro pia akazungumza kwa njia ya simu kwenye kipindi cha Power Break fast kinachorushwa na chombo cha habari cha Clouds fm