- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MAKONDA ALANIWA NA KILA TAASISI ( TLS, LHRC, TEF)
Dar es salaam: Kwa sasa jina la MAKONDA limekuwa gumzo kila sehem mwa Tanzania, Makonda, ameendelea kuwa kumzo na wadau mbalimbali wa habari nchini, huku wakimshauri Rais Dk. John Magufuli asikilize vilio vya Watanzania kuhusu kiongozi huyo. Hatua hiyo imekuja baada ya mkuu wa mkoa kufanya uvamizi katika kituo cha televisheni kinachomilikiwa na Clouds Media Group kwa lengo la kuamuru kurushwa kwa kipindi kinyume cha sheria na kanuni za uandishi wa habari.
Makonda alivamia kituo hicho Ijumaa ya Machi 17, mwaka huu saa 4:46 usiku akiwa na askari pamoja na maofisa wa idara nyeti, ambao walikuwa wamebeba silaha nzito kwa lengo la kwenda kuwatisha watangazaji waliokuwa zamu. Akizungumza jana Dar es Salaam, Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya tatu, Frederick Sumaye, amesema hawezi kushangaa mambo anayofanya Makonda endapo atakuwa amepata alama sifuri katika taaluma yake.
Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema hawezi kumtupia lawama Makonda kwa kile anachokifanya, endapo matokeo ya elimu yanayozungumzwa yana ukweli ndani yake. Alisema licha ya Rais Dk. John Magufuli kumkingia kifua kwa kusema kuwa hataki kupangiwa nani awe nani katika utawala wake, ila kama kuna mtu anakosesa ni vema akashauriwa ili aweze kufanya marekebisho.
“Kutokana na alichokifanya Makonda kuvamia Clouds Media Group na anayoendelea kulaumiwa na kulalamikiwa katika utendaji wake, hafai kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. “Rais anatakiwa kumpangia kazi nyingine yoyote itakayomfaa kulingana na uwezo wake wa kuongoza, lakini sio kuongoza Mkoa wa Dar es Salaam, hapa hapamtoshi kabisa,’’ alisema Sumaye.
Alisema kinachotokea kwa sasa kinaitwa ‘Level of incompetence’, hapo ndiyo kiwango chake cha mwisho, haiwezekani Mkoa wa Dar es Salaam ukategemea maajabu zaidi ya anayofanya Makonda. Sumaye alihoji kauli ya juzi ya Rais Magufuli kwa kusema kwamba alichukua fomu yeye mwenyewe, huku akimtaka kukumbuka kuwa wananchi ndio ambao walimpigia kura hadi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano jambo ambalo anatakiwa kuwasikiliza wanachoshauri kwake.
KITUO CHA SHERIA Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema kitendo kilichofanywa na Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds ni kosa la jinai, hivyo Serikali imchukulie hatua. Mbali na hilo, kituo hicho kimewashauri Clouds kumshtaki Makonda, huku kikivitahadhalisha vyombo vya habari kuwa na urafiki usiovuka mipaka na badala yake visimamie weledi wa kazi.
Kituo hicho pia kimemshauri Rais Magufuli kusikiliza sauti za Watanzania kwani licha ya kuchukua fomu ya kugombea urais peke yake, hakujipigia kura mwenyewe.
Akizungumza jana, Mkurugenzi wa kituo hicho, Dk. Hellen Kijo-Bisimba, alisema hatua hiyo ya Makonda inaangukia katika kosa la jinai chini ya kanuni ya adhabu ya mwaka 2002.
“Kitendo kilichofanywa na Makonda ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya uhuru wa habari na utawala wa sheria, vitendo kama hivyo vinaidhalilisha Serikali kitaifa na kimataifa kama nchi ambayo inajipambanua kuwa kisiwa cha amani. “Vyombo vya habari vipo kwa mujibu wa sheria na vinaongozwa na sheria kadhaa, ikiwamo ya huduma za vyombo vya habari ya mwaka 2016, hivyo vinapaswa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na si kuingiliwa na mtu binafsi au mamlaka,” alisema Dk. Bisimba. Kwa mujibu wa Dk. Bisimba, sheria hiyo imeeleza wazi mamlaka ambazo zinaweza kuviwajibisha vyombo vya habari pale ambapo vitaonekana vinatoa habari za uchochezi kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 49 (1) na 50 (1).
“Pale inapotokea watu binafsi au mamlaka kutumia nafasi walizonazo kutaka kushinikiza habari fulani kutolewa na vyombo vya habari kwa masilahi binafsi, ni kukiuka misingi ya sheria. “Na kama jambo hilo linafanywa na mtu mwenye mamlaka ya kuhakikisha utekelezwaji wa sheria na ulinzi wa amani katika mkoa, kwa mujibu wa sheria ya Tawala za Mikoa kifungu cha 5 (1), ni jambo la kihuni na la kupingwa kwa nguvu katika taifa linalofuata misingi ya haki na utawala wa sheria,” alisema.
#mtanznia