- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MAKALA : MAMBO KUMI USIYOYAJUA KUHUSU MSHAMBULIAJI MDOGO WA YANGA
Yohana Nkomola amekutana na Muakilishi.com na kueleza mambo 10 ambayo hakuweka wazi tangu kujulikana kwake
Yohana Nkomola ni mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya yanga,ni mshambuliaji aliyefahamika zaidi kwa namna anavyojua kuchungulia nyavu za wapinzani na kufunga mabao ya aina yake.
Ni mshambuliaji mdogo zaidi ndani ya yanga 18,akiwa na serengeti boys Yohana aliweza kufanya makubwa zaidi na kupata umaarufu wa aina yake ndani ya muda mchache.
Uwezo wake wa kufunga na kupunguza mabeki wa wapinzani wake ndiyo kivutio kikubwa kilichowashawishi mabingwa watetezi wa ligi kuu bara Yanga,kumsajili kinda huyu.
Katika maisha ya soka ya yohana yapo mambo mengi aliyopitia mpaka kufika alipo sasa ingawaje bado ana ndoto za kufika mbali,ila kujituma kuzingatia mazoezi na maagizo kwa walimu wake ndiyo nguzo bora zilizomfanya kufika yanga akiwa na umri mdogo zaidi
Yapo mambo mengi ambayo Nkomola anayapenda na kuyachukia katika maisha yake,na yapo ambayo amepitia mpaka kufika sehemu aliyopo kwa sasa,Muakilishi.com imefika nyumbani kwa mchezaji huyo na kuzungumza nae kama ifuatavyo
Mahusiano na kaka yake
Yohana ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto sita ya mzee Nkomola,miongoni mwa watoto hao sita kuna kaka yake Samweli Nkomola,anayekipiga Lipuli fc ya Iringa,pamoja na Yohana kuwa mdogo katika soka,anakwambia kaka yake Samweli hajawahi kumuhusia jambo lolote linalohusu soka,Kujituma kwake,bidii ndio nguzo iliyomfanya kufika yanga ila hajawahi kupata ushauri wa aina yoyote kuhusu soka.
Hajawahi kukutana na matukio mabaya
Anasema tangu kukua kwake mpaka leo hii,hajawahi kukutana na matukio mabaya,kwani mara zote amekuwa ni mtu wa kukaa ndani tu,marafiki wengi ni wale wenye tabia zisizofaa hivyo hakuona sababu ya kuwa na marafiki,alikuwa akirudi mazoezini anabaki ndani tu kuepuka kukutana na matukio na kashfa zingine.
Bongo anapita,lengo lake ni Ulaya
Pamoja na kufanikiwa kusajiliwa na Yanga Nkomola anakwambia lengo lake sio kucheza yanga milele,anapita tu,yanga ni kama njia,tena anakwambia inawezakana hata miaka miwili isifike akatimka kwenda nje,maana kuna timu ambazo alifanya majaribio ikiwemo Etoile De sahel Fc ya Tunisia,lengo la yohana ni kufika manchester United basi na sio vingenevyo na anakwambia atafika tu maana umri bado mdogo.
Mafanikio katika soka
Ingawaje Yohana amekataa kuweka wazi kiasi cha pesa ya kwanza kulipwa katika soka, lakini anakwambia mpaka sasa ameshanunua kiwanja ambacho kipo Mbande Mbagala,kwa ajili ya kujenga nyumba yake,hana gari wala usafiri wa aina yoyote na anaishi na wazazi wake
Aina ya Marafiki asiowataka
Kama unataka kuwa rafiki wa Yohana basi hakikisha hutumii Pombe,Sigara,wala Bangi hapo ndiyo mtawezana,anasema hawezi kuwa na urafiki na mtu anayetumia vilevi vya aina hii kwa sababu yeye pia hatumii na hafikirii kutumia hata siku moja
Aina ya vyakula anavyopenda
Usije ukahisi anapenda chipsi au vyakula vya kizungu,kwake hivyo vinampitia kushoto kabisa,ukitaka kumualika huyu jamaa usipate shida andaa ubwabwa na nyama,yani hapo mpigie simu ukiona kakataa ujue yupo kambini na yanga yake.
Rafiki mkubwa wa Yohana
Mchezaji ambaye anamkubali zaidi tanzania na ndiye rafiki yake mkubwa bongo ni kipa wa yanga Ramadhan Kabwili,anasema ni rafiki yake ambaye wamehangaika wote katika harakati za kisoka mpaka leo wamefika sehemu moja,Yohana na Kabwili wameanza kufahamiana tangu 2013 na hapo ndipo walipoonza rasmi harakati za kutaka kucheza soka la kulipwa.
Wachezaji anaowakubali nje ya bongo
Yohana hana mtu maalumu ambaye anamuiga kwa vitu fulani isipokuwa anasema mtu yoyote anayefanya vizuri basi huwa anapenda kumuiga,lakini anadai anamkubali sana Mbwana Samatta na Cristiano Ronaldo wa Real madrid,kwani mara nyingi anaiga vitu fulani kutoka kwao ambavyo vinaweza kumsaidia kwa kiasi fulani
Laptop ndiyo ugonjwa wake mkubwa
Anakwambia hakuna kitu ambacho anakipenda kama kuchezea kompyuta aina ya Laptop,mara nyingi anapenda kuchezea aina hiyo ya kompyuta na kazi kubwa anayoifanya ni kucheza (video football games) na kwakuwa kwenye Pes 2018 kuna baadhi ya timu za bongo anakwambia Ngoma,Tambwe nje,na anajiweka yeye nafasi ya ushambuliaji ili aweze kutikisa nyavu za wapinzani.
Yohana hana makundi ya ajabu
Tambua kua ni mchezaji ambaye anajitambua vilivyo hivyo kwa kuwa rafiki yake mkubwa ni kipa Ramadhan Kabwili,basi asipokuwepo huwa hana sehemu yakwenda na hana makundi ya ajabu ajabu