Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 10:30 pm

LISSU: NIKIONANA NA RAIS MAGUFULI NITAMPA VIDONGE VYAKE.

Dar es salaam: Mbuge wa Singida Mashariki na Rais wa chama cha wanasheria Tanganyika TLS Tundu Lissu ameomba kuonana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli ili kujadili maswala ya Utawala wa sheria na Rais huyo, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA alisema kuwa ameomba appointment na Rais Magufuli Ili wapate kufahamiana vizuri kwani ni "mazungumzo kati ya Rais na Rais" alisema

Akihojiwa na mwananchi Lissu alisema kuwa “Nikifika nitaanza kwa kumshukuru Rais kwa kuwafundisha Watanzania maana ya utawala wa sheria, uhuru wa mawazo, uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa Mahakama na Bunge, kwa sababu ya namna anavyoendesha nchi"

Lissu Alisema kuwa wanajua kuwa Rais anamambo mengi, lakini wanatarajia atatenga muda kwa ajili TLS.

“Tunafahamu yuko busy, lakini kama anaweza kuangalia Shilawadu, atakuwa na muda hata nusu saa au saa nzima ya kuongea na kiongozi wa chama cha mawakili wa Tanganyika,” alisema.


Pia Lissu alielezea hisia zake kuwa anakwenda kumpa Rais Vidonge vyake kwa namna anavyo iendesha nchi,

“Nakwenda kumpa vidonge vyake, kabisa! Wala sitammezea. Nitamwambia kwa heshima zote kwamba Mheshimiwa Rais, sisi kama mawakili wa Tanganyika tuna wasiwasi mkubwa na mwelekeo wa Serikali yako,” alisema.


“Wamenituma nikueleze mwelekeo na matendo ya Serikali yako. Unatawala vibaya, nje ya Katiba, wameniambia nije nikwambie ujirekebishe. Nakwenda kumsimanga tu. Halafu tukitoka pale namwambia Mheshimiwa Rais tupige picha, wajue nilikuja.”