- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
KILELE CHA MALKIA WA NGUVU KILIHITIMISHWA KWA STAILI HII
Dar es salaam: Kampeni maarufu ya malkia wa nguvu ambayo iliiyo asisiwa na kuendeshwa na taasisi ya Clouds Media Group ( CMG), ikiwa na lengo la kutambua juhudi za wanawake katika nyanja mbalimbali za maisha na kuwatambulisha kwenye jamii kwa upana zaidi ili kuongeza thamani ya kazi zao za kibunifu, ili hatimaye iwe ni mfano kwa wengine katika jamii. Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere uliopo posta, mgeni rasmi akiwa ni naibu spika wa bunge Dkt. Tulia Ackson, ambaye aliambatana na viongozi wengine kama mh. Mwigulu nchemba waziri wa mambo ya ndani, Mh. Ally Happi mkuu wa wilaya Kinondoni, Mh. Sophia Mjema mkuu wa wilaya ya Ilala na Bw Ruge Mutahaba ambaye ni mkurugenzi mkuu wa vipindi clouds media group. kauli mbiu ya kampeni hiyo ni Malkia wa nguvu, mchapakazi na mbunifu.
Takribani tuzo sita zilikuwa zikiwaniwa na kutunzwa kwa washindi kadhaa kwa kila sekta pendekezwa,
Ifuatayo ni orodha ya vipengere na miongoni mwa washindi.
Sayansi na teknolojia-Consolata Lihepa
Kilimo biashara-Cecilia chambaka
Mwanamke mhamasishaji-Sophia Mbeyela.
Afya-Celina Letara
Usambazaji na mauzo ya rejareja-Latifa mohamed.
Tuzo ya heshima-Bi. Mwanaidi mayowela.
Malkia wa nguvu katika picha ya pamoja.
Shinda hilo halikwenda kàvu kavu pomoja na uwepo wa viongozi mbali mbali lakini pia mastaa wa muziki hawakukosa na mastaa waliohudhuria katika tukio hilo na wengine kupata nafasi ya kutumbuiza ni kundi la Weusi, Saida Karoli, Khadija kopa, Katarina wa Karatu (mchekeshaji),Jokate Mwegelo na wengine kama mwanasaikolojia Dkt. Ellie V.D waminiani.Baadhi ya washiriki wakiwa na tuzo zao
Pia tukio hilo lilikuwa likifuatiliwa kwa karibu kabisa na Rais wa Jamhuri muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli.