Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 7:30 pm

KAMANDA MUROTO: TUKUO LA KUUAWA M-KITI BAWACHA HALIHUSIANI NA SIASA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto, amesema tukio la kuuawa kwa Mwenyekiti wa BAWACHA Kata ya Palanga Asia Said, aliyechomwa na mshale usiku wa kuamkia leo halihusiani kabisa na siasa, bali ni kuwa mume wa marehemu huyo alikuwa na ugomvi na mtuhumiwa aliyefanya mauaji hayo baada ya kuingiza mifugo kwenye shamba lake.

Akiongea hii leo Julai 23, 2020 baada ya tukio hilo Kamanda Muroto amesema kuwa tayari jeshi hilo limemkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Mwenyekiti wa Baraza la wanawake Chadema Kata ya Palanga.

Muroto amesema Bi Asia alichomwa mshale huo majira ya usiku wakati akiandaa chakula cha jioni yeye na mume wake.

chanzo cha mauaji hayo ni mume wa marehemu anayejulikana kwa jina la Hassan Masale, kuwa na ugomvi na mtuhumiwa Haruna Ally, baada ya kuingiza mifugo kwenye shamba la Alizeti la mtuhumiwa wa mauaji ya mkewe.

"Tukio limetokea jana majira ya saa 2 usiku na alifariki baada ya kufikishwa Hospitali ya Kondoa, na Mshale uliotumika umekamatwa na mtuhumiwa amekamatwa na amekiri kufanya tukio hilo", amesema Kamanda Muroto.

Kamanda Muroto ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo alifanya tukio hilo kwa lengo la kulipiza kisasi na ndipo alipomvizia mume wa marehemu wakati akiwa nje ili kumchoma mshale na kisha mshale huo kumpata mwanamke badala ya mwanaume.