- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
Huyu ndiye Rais mpya nchini Somalia baada ya uchaguzi wa jana
Waziri mkuu wa zamani mwenye uraia wa Somalia na Marekani Mohamed Abdullahi Farmajo, amechaguliwa kuwa rais mpya wa Somalia jana. Uchaguzi huo wa kihitoria ulighubikwa na hofu ya mashambulizi ya kundi la itikadi kali la Al-Shabaab, na uliwashirikisha wabunge tu badala ya wananchi kwa ujumla.
Wajumbe wa mabaraza yote ya bunge walipiga kura zao katika kituo cha zamani cha jeshi la anga kilichokuwa na ulinzi mkali, katika mji mkuu Mogadishu, huku uwanja wa ndege wa kimataifa ukifungwa kabisa. Maelfu ya Wasomali walimiminika mitaani na kuimba jina la rais huyo mpya, huku wanajeshi waliokuwa wanashangilia wakifyatua risasi hewani. Rais mpya anawakilisha kizazi cha Wasomali waliotawanywa nje ya Somalia na mgogoro, lakini ambao wameanza kurejea nyumbani kwa tahadhari kusaidia ujenzi wa taifa lao. Wengi wa wagombea katika uchaguzi huo wana uraia wa nchi mbili.