- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
Hizi ndizo faida za kula matunda mwilini
Matunda yana faida nyingi sana za kiafya mwilini. Ukiachana na ladha tamu inayotokana na kula matunda, kila mtu anashauriwa ale matunda tofauti yasiyopungua matano (5) kwa siku ili kupata faida zote mwilini. Faida kuu za matunda ni kuzuia maradhi, kurutubisha kinga ya mwili, kupunguza sukari kwenye damu, kuleta nguvu na kuleta mafuta asilia kwenye mwili.
Watu wanaopendelea kula matunda na mboga za majani kama sehemu yao kubwa ya mlo wa kila siku hujenga kinga madhubuti za mwili dhidi ya magonjwa. Matunda yana virutubisho asilia ambavyo ni mahususi katika kujenga mwili na kuufanya kuwa na afya njema. Matunda hubeba virutubisho muhimu kama potasiam, vitamin C, vitamin A, nyuzi nyuzi (fiber) na folic acid.
Ulaji wa matunda unasaidia mwili kupata faida zifuatazo:
1.Yanapunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kiharusi.
2.Yanakinga mwili dhidi ya aina za saratani.
3.Nyuzi nyuzi (fiber) za kwenye baadhi ya matunda kama maembe zinasaidia kulinda dhidi ya magojwa kama mshituko wa moyo (heart attack), fetma na kisukari.
4. Lakini pia inasaidia kupunguza madhara ya uvimbe unaotokana na kuwa na chumvi nyingi mwilini.Kula matunda yenye potasiam kama ndizi na apricot kwa wingi yanasaidia kupunguza magonjwa ya shinikizo la damu.
5.Matunda aina hizi husaidia pia kupunguza mawe kujaa kwenye figo.
6.Vitamin C ni muhimu katika mwili kwasababu inasaidia ukuaji na utengenezaji wa tishu za mwili. Mfano ni meno na fizi. Vitamic C inasaidia pia uchocheaji wa uponaji wa vidonda kwa haraka.
7.Vitamin C inapatikana kwenye matunda mengi machachu, mfano machungwa, limao n.kFolic acid inasaidia kutengeneza chembe hai nyekundu za damu mwilini.
8.Wanawake wajawazito au walio kwenye umri wa uzazi wanashauriwa sana kula vyakula vyenye folic acid kwa wingi ili kusaidia ukuaji wa mototo tumboni na kudhibiti dhidi ya magonjwa.