- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
HANSCANA: SIHUSIKI KUMONGELEA JAMBO LOLOTE LINALO MUHUSU DARASSA
Dar es salaam: Mkali wa kuongoza video za muziki wa Bongofleva, Hancana amesema kuwa yeye si msamaji wa Darassa hajawahi kumsimamia kazi zake za sanaa hapo awali bali yeye alikuwa anamfanyia production ya muziki tu katika kazi ambazo aliwahi kufanya kwake.
"Sihusiki kuongelea jambo lolote linalo muhusu Darassa kwasababu yeye ni 'brand' na mimi sio msemaji wa 'brand' ya Darassa bali mimi ni rafiki tu. So kama yeye ni 'brand' inabidi ajitokeze mwenyewe na kujizungumzia yeye kama yeye. Haitakuwa sahihi Hancana kuzungumzia brand ya mtu mwingine", amesema Hancana.
Akizungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV leo Mai 10 baada ya mashabiki wake kudai kuwa huenda Hascana anahusika na kumsimamia kazi za Darassa huku wengine wakienda mbali zaidi kuwa pia anafahamu chanzo cha kupotea msanii huyo katika 'game' ya muziki.
Hancana amempongeza Darassa kwa kuweza kuhimili miki ya vitu vyote ambavyo watu walikuwa wanampakazia hasa kuhusu kujihusisha na dawa za kulevya.
"Nadhani hizi skendo huja kumpanikisha mtu ili wapate kumsikia anasemaje, 'sometimes' hivyo vitu vipo. Ninachomshukuru Darassa au kumpongeza ni amekuwa 'very strong' amesimama kwenye mipango yake anayoiamini 'no matter what', watu wanampanikisha kwamba anatumia dawa za kulevya mara amepotezwa kwenye muziki", amesema Hancana.