- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BURUDANI : CHID BEENZ HAJUTII MAISHA YA MADAWA YA KULEVYA ALIYOPITIA ADAI MASHABIKI WANA NAYE
MKALI wa muziki wa nchini Rashidi Makwiro,Chid Benz amesema licha ya kuzama katika matumizi ya dawa za kulevya hakuna anachojutia katika maisha yake.
Muimbaji huyo alisema kutokana na mashabiki wake kuwa bega kwa bega kwenye shida na raha,hana sababu ya kujutia kwa yale yanayomtokea.
Akizungumzia hilo kwenye mahojiano mafupi na Wasafi Tv alisema hapendi kuongelea masuala ya madawa kwani mambo hayo yameshapita.
“No!no!,tusiongelee mambo ya madawa maisha ndio yapo hivyo,hamna kitu ninachojutia siwezi kujutia nilikolabo na wasanii,siwezi kujutia yaliyonikuta,siwezi kujutia mabadiliko yangu, siwezi kujutia chochote kilichonipata,” alisema Chid Benz.
Alisema mashabiki wake wamekuwa wakimuunga mkono hata pale anapotangaza kufanya shoo mikoani,hivyo kwa sababu hiyo hawezi kujutia.
Katika hatua nyingine Chidi Benz alisema karibia studio zote alizoanya kazi kuna nyimbo zaidi ya saba hivyo muda wowote atatoa wimbo