- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BURUDANI : BUSHOKE AMTETEA Q CHILLAH ADAI HAWEZI KUKOSA SEHEMU YA KULALA
BUSHOKE : Q Chillah hawezi kukuosa sehemu ya Kulala,nizushi tu
-Adai Q Chillah hata Nairobi anaweza kulala
-Akanusha kulala Kwake
-Hajalia
MKONGWE wa muziki nchini 'bushoke'amemtetea rafiki yake ambae pia ni msanii mwenzake Q-chillah na kusema kuwa sio kweli kuwa aliwahi kulala kwake kwa sababu ya hali ngumu ya maisha.
Juzi kuliibuka tetesi kuwa Q chillah alienda kulala nyumbani kwa Bushoke kutokana na msanii huyo kuwa na hali ngumu ya kimaisha,jambo ambalo Bushoke alikanusha.
Akizungumza na EATV Bushoke alikanusha taarifa hizo na kusema kuwa sio kweli kuwa rafiki yake alienda kujihifadhi kwake baada ya kuachana na Mwanamke wake.
"Q-chief hajawahi kuja kukaa kwangu na ikitokea anakaa kwangu basi ujue kaja kupiga stori tu na sio kwamba ana shida ya kulala,"alisema Bushoke
Alisema Q chillah hawezi kukusa sehemu ya kulala,kwani anauwezo wa kulala hata nje ya chini na ikitokea kulala kwake basi ni maamuzi yake mwenyewe kuchagua anapopataka.