- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BURUDANI: BEYONCE NA JAY Z WATOA ALBAM YA PAMOJA TRUMP ATAJWA
Baada ya kuwepo kwa tetesi nyingi juu ya Beyonce na mumewe Jay-Z kutoa albamu yao ya pamoja hatimaye wamefanya kitu hicho
Albamu hiyo imepewa jina Everything is Love (Kila Kitu ni Mapenzi).
Albam hiyo inapatikana katika huduma ya kusikiliza na kununua nyimbo mtandaoni inayomilikiwa na Jay-Z kwa jina Tidal.
Beyonce alitoa tangazo la kutolewa kwa albamu hiyo akiwa kwenye jukwaa London na wawili hao waliwashukuru mashabiki wao kwa kujitokeza kuwatazama wakati wa tamasha yao ya kuizuru dunia.
Alisema: "Kwa sababu twawapenda sana, tuna kitu cha kipekee sana kwa ajili yenu."
Video ilichezwa kwenye skrini na mwishowe kukatokea ujumbe kwamba 'ALBAMU IMETOKA SASA'.
Video ya muziki ya dakika sita ilitolewa punde baadaye, ambayo iliandaliwa katika makumbusho maarufu duniani ya Louvre mjini Paris.
Hiyo ndiyo albamu yao ya kwanza wakiwa pamoja na imeelezwa kama video ya kusherehekea ndoa ya na asili yao kama watu weusi.
Katika abamu ya karibuni zaidi aliyokuwa ameitoa Beyonce akiwa peke yake kwa jina Lemonade mwaka 2016, alikuwa amezungumzia kutoaminika katika ndoa.
Mwaka mmoja baadaye, Jay-Z alitoa albamu yake kwa jina 4:44.
Kwenye albamu hiyo, alizungumzia kuomba msamaha.
Mashabiki wa wawili hao wamefurahishwa na tangazo la albamu hiyo, baadhi wakilinganisha maisha yao na mchezo wa kuigiza, na kwamba hii ni sura ya tatu.