- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BURUDANI : ALIKIBA AFUNGUKA KUWA ALIVYOKUTANA NA AMINA AKAJUA TU NDIYE MKE SAHIHI
Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka kwa mara ya kwanza kukutana na mke wake Bi. Amina Khalef alijua wazi kuwa ndiye mwanamke wa kuoa.
Kwenye Interview Baby kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm, Amina ameweka wazi kuwa yeye na Ali kiba walikutana Kwenye ndege na wakabadilishana namba na kuwa marafiki:
Mara ya kwanza kukutana na ilikuwa kwenye ndege na hatukuzungumza mara ya pili Kaka yangu binamu ndiyo alinikutanisha nae maana walikuwa marafiki sana na hapo ndiyo tulianza urafiki wetu kabla ya kufika hapa tulipo“.
Hata hivyo, Bi. Aminah amesema kuwa Alikiba ndiye aliyeanza kumtamkia kuwa anampenda na yeye akamwambia kama ni kweli aende kwa wazazi wake akajitambulishe.
Ali Kiba na yeye ameweka wazi kuwa alivyokutana na Bi Amina mara moja akajua yule ndio mke wa kuoa hivyo mara moja akamfuata gavana wa Mombasa Joho akamwambia anataka kuoa.Yeah Joho ni mtu ambaye aliniongoza sana kwenye maswala ya msingi, kama nilivyokuwaambia kwenye maswala ya dini, mimi na mke wangu tulikutana Nairobi, tukajuana tukaanza kuwasiliana.
Tulivyokuwa marafiki na Hassan nikamwambia kaka kuna msichana anakaa hapa, akaniambia kama ni kuoa basi process zifuatwe nilipoonja Mo Faya tu!, nikaoa hapo hapo,