- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BURUDANI: ALICHOKIZUMZA ALIKIBA KUHUSU KESI YAKE YA KUTUNZA MTOTO
Dar es salaam: Msanaa Nyota nchini Tanzania Ali saleh Kiba maarufu kama ALIKIBA amesema kuwa hajui dhamira ya mama wa mtoto wake Hadija Hassan kufungua kesi hiyo kwa sababu kama ni matunzu kwa baba anatekeleza.
Akizungumza Leo Mei 11 katika kipindi cha 360 kinachorushwa na CloudsTV, Alikiba amesema kesi hiyo imefunguliwa kwa nia ya kumkomoa. “Simuelewi kwa nini amefungua kesi kwa sababu kama ni mtoto namtunza.
Kiba amesema ugomvi mkubwa unakuja pale familia yetu inapotaka kumchukua mtoto. Inapotaka kukaa naye japo kwa siku chache, hataki,” amesema. “Jambo hilo kwa kweli linatutia wasiwasi sana, tunajiuliza kwanini anafanya hivyo.” Amesema mpaka sasa hajapata barua ya wito huo mahakamani na kuahidi kuendelea kumtunza mtoto huyo ambaye katika siku za karibuni alimuhamishia ‘shule za bei mbaya’.
watoto wa Alikiba
Alipoulizwa idadi ya watoto wake alionao kwa sasa, Alikiba amesema anao watatu, wawili wa kike na mmoja wa kiume.
Hadija ambaye pia ni Mfanyabiashara wa nguo za mitumba jijini Dar es Salaam alidai kuwa alijifungua mtoto huyo aliyezaa na Ali Kiba mwaka 2013 katika hospitali ya Mikocheni jijini Dar es Salaam na kwamba hadi sasa mtoto huyo hapati matunzo stahiki kutoka kwa baba yake.
Hadija ameiomba Mahakama kuamuru msanii Ali Kiba awe analipa kiasi cha sh 1.41 milioni kwa mujibu wa sheria, akirejea sheria ya watoto ya mwaka 2009.
Hadija alieleza mchanganuo wa kiwango hicho cha fedha, alisema kuwa kwa mujibu wa sheria, “Ali Kiba anapaswa kutoa huduma kila mwezi, chakula sh 150,000, matunda sh 50,000, chakula cha ziada sh. 50,000, michezo na burudani za watoto sh. 100,000, nguo sh. 60,000 na matibabu shilingi 50,000.”
Alisema mbali na huduma hizo tajwa zinazopaswa kutolewa kila mwezi, anaiomba mahakama hiyo kumuamuru mlalamikiwa kutoa sh 950,000 kama ada shule kwa muhula mmoja.
Hadija amefungua kesi hiyo akisaidiwa na Kituo cha Wanawake cha Msaada wa Kisheria (WLAC).